Monday, 6 August 2012

malema foundationDescription: C:\Users\Mwalimu Marwa\Desktop\MAREMA.jpg         MAREMA
      FOUNDATION

TAARIFA YA KIKAO CHA KWANZA CHA MALEMA FOUNDATION TAREHE 15 JULY 2012.
MAHUDHURIO
S/N
JINA KAMILI
CHEO
NAMBA YA SIMU
1.
Mzee Samwel Marwa
MJUMBE

2.
Mama Chacha
MJUMBE

3.
Mzee Daniel Marwa.
MJUMBE

4.
Mama Mwita
MJUMBE

5.
Charles Marwa
MJUMBE

6.
John Shadrack
MWENYEKITI

7.
Joshua Marwa
MHAZINI

8.
Mama Samwel
MJUMBE

9
Zakaria Shadrack
MJUMBE

10
Mrs Zakaria Shadrack
MJUMBE

11
Peter D. Marwa
MJUMBE

12
Mama Vick
KATIBU MSAIDIZI

13
Daudi Samweli
MJUMBE

14
Marema Samwel
MJUMBE

15
Mrs Marema
MJUMBE

16
Seba J. Marwa
M/KITI MSAIDIZI

17
Mama Mary
MJUMBE

18
Thomas Daniel
KATIBU

19
Petro Shadrack
MJUMBE

20
Rhobi Shadrack
MJUMBE

21
Shila Samwel
MJUMBE


AGENDA

A.    Kuanzisha umoja wa Familia ya MarSwa Nyambari na Kuanzisha mfuko wa Familia.
B.     Kujadili hali ya ugonjwa wa Mzee Daniel Marwa na Mustakabali wa  Afya yake.
C.     Kujadili hatma ya Watoto wa Musa Jones walioachwa na mama yao Ester Musa kwa Mzee Marwa.
D.    Mengineyo.

MUHTASARI WA KIKAO

Wajumbe walifungua kikao kwa Ombi kutoka kwa Mama Mwita na baadae Mzee Marwa aliweka wazi kusudi la kuitisha kikao.
Kabla ya kuanza kujadili agenda zilizowekwa mbele ya kikao wajumbe walianza kwa kupendekeza majina ya viongozi ambapo wafuatao walipendekezwa na kupitishwa.
1.      John Shadrack                      Mwenyekiti
2.      Seba J Marwa                       Mwenyekiti Msaidizi
3.      Thomas Daniel                     Katibu
4.      Libe  Peter (Mama Vick)     Katibu Msaidizi
5.      Joshua Marwa                      Mhazini


AGENDA 1   KUANZISHA UMOJA WA FAMILIA YA MARWA NYAMBARI NA KUANZISHA MFUKO WA FAMILIA.
Wajumbe walikubaliana na wazo la kuwa na Umoja wa Familia ambapo jina MAREMA FOUNDATION lilipendekezwa na kupitishwa.
Kuhusu Mfuko wa Familia Wajumbe walikubaliana na wazo hilo na kuazimia yafuatayo
a.      Kiingilio
kiwe sh 50,000 kwa kila mwanafamilia (kwa wale wenye ndoa kila mwanandoa anatoa kiingilio chake)
b.      Ada
Ada ilipendekezwa sh 10,000 kila mwezi kuazia Januari 2013. Lakini kuanzia August 2012 – Disemba 2012 ada itakuwa sh 5000


AGENDA 2.   KUJADILI HALI YA UGONJWA WA MZEE DANIEL MARWA NA MUSTAKABALI WA  AFYA YAKE.
Agenda ya pili ilikuwa kujadili afya ya Mzee Danieli kwa kuangalia historia ya tatizo lake na matibabu yake.
Ø  Ilionekana matibabu yaliyokwisha fanyika yamesaidia kwa kiasi kikubwa.
Ø  Historia ya ugonjwa na taarifa ya daktari kutoka kwa Mzee Marwa ilibainisha kuwa chanzo halisi cha tatizo kilikuwa ni msongo wa mawazo (stress)
Ø  Wajumbe walikubaliana namna ya kumsaidia Mzee katika yafuatayo.
.1.       Wajumbe walikubaliana asaidiwe chakula kwa miezi kadhaa
.2.       Viongozi walipewa jukumu la kuandaa bajeti yake ya mwezi na kuileta katika kikao kijacho.
.3.       Wajumbe walitoa mchango wa papo hapo kusaidia kwa muda huo bajeti ikingojewa na sh 22,000 zilipatikana.

AGENDA 3. KUJADILI HATMA YA WATOTO WA MUSA JONES WALIOACHWA NA MAMA YAO ESTER MUSA KWA MZEE MARWA
Ø  Taarifa fupi kuhusu watoto hawa Jane na Happy ilisema kuwa watoto hawa waliachwa na mama yao (Ester Musa) katika nyumba waliyokuwa wakiishi na baada ya siku nne (kwa ushauri wa majirani) wakaamua waende kwa babu yao Mzee Marwa.
Ø  Watoto walirudi nyumbani baada ya kupewa taarifa isiyo rasmi kuwa mama yao amerejea nyumbani lakini walipoenda hawakumkuta. Majirani waliwapeleka kwa njumbe wa shina ambaye aliwapeleka kwa Mwenyekiti wa mtaa na baadaye wakapelekwa polisi.
Ø  Polisi wakaamua kuwapeleka tena kwa mzee Marwa ili watunzwe wakati mama yao (Ester Musa) alitafutwa.
Ø  Wajumbe walipendekeza Ester Musa (mama wa watoto hawa) atafutwe kikao kijacho ili upatikane muafaka kuhusu watoto hawa.

KUFUNGA KIKAO
Wajumbe walikubaliana kukutana jumapili ya Kwanza ya kila Mwezi.
Wajumbe walifunga kikao kwa kupata ombi kutoka kwa Charles Marwa na kutawanyika.

No comments:

Post a Comment